Hii ni habari njema kwa wapenzi wa Tecno, HiOS program endeshi mpya kutoka Tecno inayokuja kubadilisha mwenekano wa simu kutoka kampuni hii.
Tumezoea kuona kampuni kama Samsung, HTC na LG wakija na matoleo yao ya program endeshi yanayofanya kazi juu ya program mama ya Android. Kampuni ya Tecno imekuja na toleo jipya kabisa la program endeshi yake itakayokuwa inafanya kazi juu ya program mama ya Android huku ikiwa na vingi vitakavyofanya matumizi ya simu hizi kuwa ya starehe zaidi.
Kwa watumiaji wa Tecno C8 tayari wameshaanza kupakua toleo la majaribio la HiOS kwa mujibu wa mtandao wa tecnospot japokuwa
toleo kamili la mfumo endeshi huu mpya kutoka Tecno utatoka hapo April.
Inasemekana simu mpya kutoka Tecno ya Tecno J8 itakuwa simu ya kwanza
kutoka na HiOS na itatoka rasmi mwezi wa pili. Kama ilivyoandikwa katika
mtandao wa tecnospot hapo chini,
“HiOS Ni nini? Ni mfumo wa Android wa
uendeshaji katika simu ya mkononi ulioongezwa na kuboreshwa kwa ajili ya
watumiaji wa simu za smartphone za TECNO. Kama ni mntumiaji wa simu ya
TECNO C8, tuna kutaajabisha/kushangazi mtumiaji, pakua (download) TECNO
C8 Hi-Manager Upgrade. HiOS ni toleo zuri la kuifaya TECNO iwe ya pekee,
nadhifu na ya kufurahisha”
Baadhi ya picha za mfumo huo mpya tayari
zimevuja mtandaoni na wadau wanasema tecno wamekuja kufanya mapinduzi ya
soko la smartphones. Toleo la kwanza linalopatikana sasa lina ukubwa wa
40MB na limeanza kutolewa kwa njia mbili, ile ya kupakua moja kwa moja
kwa kutumia simu yako (OTA Update) na lile la kuupdate kwa kutumia
memory kadi yako (diski hifadhi)
1. OTA upgrade (recommended)
Kifurushi cha moja kwa moja (kinapendekezwa)
http://bit.ly/1RxDlCH 2. Kifurushi cha kutumia Tcard (memory card) kwa toleo namba C8-H352-A2-L-20160118
http://bit.ly/1RxDjL5
3. Kifurushi cha matoleo mengine kwa kutumia Flash Tool
http://bit.ly/1RxDohZ
Nini kipya kitakuja na HiOS?
- Device Optimizer (Kiboresha shughuli)
- Kivinjari kipya cha Tecno Browser kilichotengenezwa kwa misingi ya Chromium
- Kicheza muziki kipya (music player) kikiwa na machaguo mengi ya sura (skinns)
- Na mengine mengi tu kutoka Tecno